Swahili

Read the translated rules below or download a PDF

Kategoria za Mpiga Picha wa Mwaka wa Viumbe-mwitu

Wanyama katika Mazingira yao

Kuleta hisia ya mazingira ya anga na hisia ya sehemu – ikiwa na makazi asili kama sehemu kuu ya picha - kuonyesha jinsi mnyama ni sehemu ya lazima ya mazingira yake.

Picha za Wanyama

Za kuonyesha sifa pambanuzi za kiumbe mmoja au kundi mwandani la wanyama kwa njia ya kuchochea mawazo au kumbukumbu.

Tabia: Amfibia na Watambaazi

Za kuonyesha tabia hai ambayo inaongeza ufahamu wetu juu ya asili ya spishi.

Tabia: Ndege

Za kuonyesha tabia ya kukumbukwa, isiyo ya kawaida au yenye kuchochea hisia.

Tabia: Wasouti wa mgongo

Za kuonyesha tabia ya kuvutisha fikra au ya kukumbukwa ya kaumu ya wanyama wadogo wasouti wa mgongo - wawe wa ardhini, hewani au majini.

Tabia: Mamalia

Za kuonyesha tabia ya kukumbukwa, isiyo ya kawaida au yenye kuchochea hisia.

Bahari – Mtazamo kwa Mapana

Kuripoti juu ya ushawishi muhimu na umuhimu wa mazingira ya bahari kwetu sisi au kwa sayari. Picha zinaweza kuchukuliwa juu au chini ya maji. Zinapaswa kuwa na ujumbe - wa kiishara au halisi - wa bahari kama mabwawa ya mengi ya ajabu au bahari kama viendesha tabia nchi na hali ya hewa, au kama mifano ya jinsi binadamu wanavyotumia mbaya, linda au rejesha mazingira ya bahari.

Mimea na Kuvu

Kuonyesha asili ya mmea au kuvu au kuonyesha umuhimu au kazi wake katika mazingira yake au njia zake za kuendelea kuishi.

Sanaa ya Kiasili

Zinazofananisha uzuri mwepesi au sanaa changamani ya mazingira asilia. Picha zinaweza kuwa za rangi au nyeusi na nyeupe na ingawa zinaweza zisifanane na vigezo vya kategoria nyingine, lazima zibaki kuwa za kimazingira asilia.

Ndani ya Maji

Za kuonyesha maisha ya majini, iwe mazingira ya baharini au maji baridi. Picha zinaweza kulenga tabia ya wanyama au kuonyesha wanyama au mimea kama sehemu ya mazingira ya majini.

Viumbe-mwitu vinavyoishi Sehemu Waishizo Binadamu

Kwa kulenga jinsi viumbe asilia vinavyomiliki au ishi pamoja kwenye mazingira yaliyo zaidi na wanadamu, iwe ni kunasa maajabu ya maisha ya kila siku au yale yasiyotarajiwa au yasiyoonekana kwa kawaida.

Mbuga Kinamasi – Mtazamo kwa Mapana

Kueleza umuhimu wa mifumo ya ikologia ya maji baridi, kuanzia vilele vya milima na mboji za nyanda za juu, mito na maziwa hadi kwenye delta, mabonde ya mafuriko, maziwa ya tope na mikoko. Picha zinaweza kuwa na msukumo wa kuvutia kupitia athari au uzuri wake au kuonyesha simulizi ya mazingira au uhifadhi ambayo inaonyesha umuhimu wa mbuga kinamasi kwa mazingira asilia na / au watu.

Uandishi wa Habari Kupitia Picha

Kuchunguza uhusiano kati ya wanadamu na ulimwengu wa asilia. Picha zinaweza kuwa za kuchochea, kuinua, kuchochea fikira au kufunulisha, na inapaswa kuonyesha jinsi mitazamo, maamuzi na matendo yetu yanavyoathiri ulimwengu asilia.

Tuzo la Uandishi wa Habari Kupitia Simulizi kwa Picha

Zikisimulia hadithi ya nguvu, picha hizi sita hadi kumi zinapaswa kuwa na ubora wa kibinafsi na uthabiti wa pamoja kiusimulizi. Hadithi zinaweza kuwa za kuchochea, kuinua, kuchochea fikira au kufunulisha na zinafaa kuonyesha jinsi mitazamo, maamuzi na matendo yetu yanavyoathiri ulimwengu asilia. Wasilisha hadithi zenye picha hadi 10, ambazo baraza la waamuzi litachagua zisizozidi sita.

Tuzo la Nyota ya Kesho (kati ya umri wa miaka 18 hadi 26)

Kuonyesha mtindo na dhamira ya kisanii, sampuli hii ya picha bora kabisa za mpiga picha (picha sita hadi kumi zinazohusu vitu au mitazamo tofauti) unapaswa kuonyesha upana wa ustadi na maono lakini wenye ubora thabiti kila mara.

Tuzo la Jalada la Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu (umri wa miaka 27 na zaidi)

Kuonyesha sampuli ya kazi bora kabisa ya mpiga picha, picha hizi (sita hadi kumi) zinapaswa kuendana pamoja vizuri, iwe kupitia mtindo au mtazamo fulani au kulenga mada fulani, lakini hazihitaji kusimulia hadithi moja.

Masharti ya Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka

Tafadhali zingatia kuwa kuingia kokote katika Shindano la Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka papo hapo kutakuwa chini ya Masharti haya. Kama ukiingia, wewe mshindani ("wewe") lazima usome na uwajibike na Masharti haya kwani yanatengeneza mkataba wa kisheria kati yako na Natural History Museum Trading Company Limited.

1. KUHUSU SHINDANO

(1) Shindano la Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka (“Shindano”) linamilikiwa na Natural History Museum Trading Company Limited ("sisi"). Sisi ni kampuni tanzu ya biashara ya bodi la kimashirika inayoitwa Trustees of the Natural History Museum (“Jumba la Kumbukumbu”). Jumba la Makumbusho ni shirika la hisani lisilotozwa kodi [charitable organisation] lililosajiliwa chini ya sheria za Uingereza. Faida tunayoipata ni ya aina ya zawadi inayotolewa kwa Jumba la Kumbukumbu na inaweza kutumika kusaidia shughuli zake ikiwa ni pamoja na bila kikomo Mashindano zaidi na utafiti wa kisayansi. Mawasiliano yoyote nasi kuhusu SShindano la Watu Wazima au Shindano la Vijana (isipokuwa kama imeainishwa vinginevyo hapo chini) yanapaswa kupitia kwenye anwani ya barua pepe: wildlifephotographeroftheyear@nhm.ac.uk.

(2) Shindano linajumuisha Shindano la Watu Wazima lililowazi kwa wapiga picha wenye umri wa miaka 18 na zaidi, na Shindano la Vijana lililowazi kwa wapiga picha wenye umri wa miaka 17 na chini.

(3) Kutangaza Shindano, picha zilizotuzwa Tuzo na Baraza la Waamuzi zinaweza kuonyeshwa katika:

(i) maonyesho kwenye Jumba la Makumbusho ya Historia ya Asili (Natural History Museum) London (“Maonyesho ya WPY” - “the WPY Exhibition”);

(ii) matoleo yafuatayo ya Maonyesho ya WPY yanayoendeshwa na wenye leseni katika nchi yoyote ("Ziara ya Maonyesho") na

(iii) maonyesho yanayoendeshwa na sisi au Jumba la Kumbukumbu kwenye eneo lolote ambalo linaonyesha picha za Mashindano ya Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka ("Maonyesho Yanayohusiana").

Katika Masharti haya, Maonyesho ya WPY, Ziara ya Maonyesho na Maonyesho Yanayohusiana kwa pamoja yatajulikana kama "Maonyesho". Fungu la 8 hapa chini linaelezea haki maalum za leseni kuhusu utumiaji wa picha zilizopewa Tuzo.

(4) Shindano na maonyesho kwenye Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili London yatokanayo ya mshindi au uwasilisho unaopendekezwa sana vinaweza kufadhiliwa na shirika ambalo litachaguliwa na sisi kwa hiari yetu pekee, ("Wa/Mfadhili Rasmi").

2. KUINGIA KWENYE SHINDANO

(1) Uwasilisho kwenye shindano lazima uwe umepokelewa ifikapo saa 11.30 asubuhi majira ya GMT, mnamo Alhamisi tarehe 9 Desemba 2021 (‘tarehe ya mwisho’).

(2) SShindano la Watu Wazima ni wazi kwa mtu yoyote aliyetimiza umri wa miaka 18 au zaidi Alhamisi mnamo tarehe 9 Desemba 2021, kasoro:

(i) watu (na wenzi wao na familia) wanaohusika katika uandaaji au uamuzi wake; au

(ii) waajiriwa wa Kampuni ya Natural History Museum Trading Company Limited, au Trustees of the Natural History Museum au Wa/Mfadhili Rasmi.

(3) Kwa kuingia kwenye Shindano la Watu Wazima, unakubali:

(i) kutii Masharti na kuhakikisha kuwa uwasilisho wako unaendana na Masharti;

(ii) kuwa na viwango vya juu kabisa katika masuala yote yanayohusiana na Shindano;

(iii) kutofanya au kusema kitu chochote ambacho kinaweza kuharibu sifa yetu au ya Shindano, Maonyesho, Jumba la Makumbusho, Wa/Mfadhili Rasmi, Mmiliki wa Leseni ya Ziara ya Maonyesho (iliyofafanuliwa katika kifungu cha 8 (5) au washindani wengine; na

(iv) kwamba utawajibika kwetu, kwa Jumba la Makumbusho na kwa Wa/Mfadhili Rasmi kwa uharibifu wowote au hasara yoyote itakayotokea kwa mashirika hayo kwa sababu ya ukiukaji wako wa Masharti.

(4) Hauruhusiwi kuwasilisha picha ambazo:

(i) zinaonyesha mifugo, wanyama vipenzi, na/au mimea ya kupanda; au

(ii) zinakiuka majukumu yoyote ya kimaadili yaliyotolewa hapa chini.

(5) Uwasilisho katika shindano wowote utakaokutwa haufuati Masharti katika hatua yoyote ya SShindano la Watu Wazima unaweza ukafutwa. Hakuna marejesho au posho zozote zitakazolewa iwapo uwasilisho utafutwa na tuzo zozote zitanyang’anywa. Ikiwa ukiukaji umetokea, lakini unagunduliwa baada ya tuzo, basi tunaweza kuondoa uwasilisho kwenye Maonyesho na / au shughuli zinazohusiana zozote na kuhitaji kurudishiwa au kurejeshwa kwa tuzo yoyote iliyopokelewa tayari. Uamuzi wetu wowote unaohusiana na Shindano ni wa mwisho na wa mujibu. Hakuna mijadala itakayozingatiwa na hatutaingia katika mawasiliano baada ya hapo kuhusu maamuzi kama hayo.

(6) Pamoja na kwamba taarifa katika Masharti haya ni sahihi, sisi, kwa hiari yetu tu lakini tukiwa tunatatenda kwa busara, tunahifadhi haki bila kutoa taarifa kabla ya:

(i) Kurekebisha Masharti bila marejesho;

(ii) Kubadilisha tuzo kwa mujibu wa kifungu cha 6 (8);

(iii) amua ikama sherehe yoyote ya tuzo ya Shindano itakuwa hafla au itafanyika kupitia mtandaoni tu;

(iv) samehe ukiukaji wa Sheria bila kurejesha; na/au

(v) kufuta Shindano na kusitisha mikataba na leseni zilizoundwa na Masharti haya kwa kuzingatia kurudishiwa ada ya kuingia kwenye shindano.

3. SHINDANO LA WATU WAZIMA – KUWASILISHA

(1) Uwasilishaji lazima ufanyike kupitia www.wildlifephotographerofyeyear.com kabla ya saa 11.30 asubuhi majira ya GMT Alhamisi mnamo tarehe 9 Desemba 2021.

(2) Ada ya uwasilishaji ya mara moja tu na ambayo haitarudishwa ya £30.00 inahitajika kutoka kwa kila mshindani inaweza kulipwa hadi saa 11.29 za asubuhi, majira ya GMT mnamo Alhamisi 2 Desemba 2021. Kuanzia saa 11.30 asubuhi majira ya GMT mnamo Alhamisi tarehe 2 Desemba ada ya mara moja tu na ambayo haitarudishwa ya uwasilishaji itakuwa £35.00 na inahitajika kutoka kwa kila mshindani. Ili kuwezesha waombaji anuwai, ambao wanaishi katika nchi zozote zifuatazo hawatabidi kulipa ada ya uwasilishaji kama wanaweza kutoa ushahidi wakiombwa kufanya hivyo: Afghanistan, Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Kamerun, Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Comoros, Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Haiti, Honduras, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Nicaragua, Niger, Nigeria, Korea Kaskazini, Papua New Guinea, Ufilipino, Rwanda, São Tomé na Príncipe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Swaziland, Syria, Tajikistan, Tanzania, Togo, Uganda, Yemen, Zambia na Zimbabwe.

(3) Shindano la Watu Wazima lina kategoria zifuatazo:

(i) Wanyama katika Mazingira yao;

(ii) Picha za Wanyama;

(iii) Tabia: Amfibia na Watambaazi;

(iv) Tabia: Ndege; Tabia: Wasouti wa mgongo;

(vi) Tabia: Mamalia;

(vii) Mimea na Kuvu;

(viii) Ndani ya Maji;

(ix) Viumbe-mwitu vinavyoishi Sehemu Waishizo Binadamu;

(x) Sanaa ya Kiasili;

(xi) Bahari – Mtazamo kwa Mapana;

(xii) Mbuga Kinamasi – Mtazamo kwa Mapana;

(xiii) Uandishi wa Habari Kupitia Picha;

(xiv) Tuzo la Uandishi wa Habari Kupitia Simulizi kwa Picha;

(xv) Tuzo la Nyota ya Kesho (kati ya umri wa miaka 18 hadi 26); na

(xvi) Tuzo la Jalada la Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu (umri wa miaka 27 na zaidi).

(4) Unaweza kuwasilisha picha zisizozidi ishirini na tano (25) kwa ujumla bila kujali idadi ya kategoria hapo juu unazowasilishia. Hii ni pamoja na:

(i) kati ya picha sita (6) na kumi (10) kwa Tuzo la Uandishi wa Habari Kupitia Simulizi kwa Picha kwa kila hadithi. Unaweza kuwasilisha hadi hadithi mbili (2) tu katika kategoria hii. picha zisizo zidi sita (6) zitachaguliwa na Baraza la Waamuzi.

(ii) kati ya picha sita (6) na kumi (10) kwa Tuzo la Nyota ya Kesho ambazo picha zisizozidi sita (6) zitachaguliwa na Baraza la Waamuzi. Unaweza kuwasilisha jalada moja (1) tu kwa kategoria hii; na

(iii) kati ya picha sita (6) na kumi (10) kwa Tuzo la Jalada la Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu ambazo picha zisizozidi sita (6) zitachaguliwa na Baraza la Waamuzi. Unaweza kuwasilisha jalada moja (1) tu kwa kategoria hii .

4. MASHARTI YA UADILIFU

(1) Ukiukaji wowote wa Masharti ya Uadilifu hapa chini utakuwa ni ukiukaji wa Masharti

(2) Picha zako lazima ziwe zinataarifia juu ya ulimwengu asilia kwa njia ambayo ni ya ubunifu na ya uaminifu na ya kimaadili:

(i) uwasilisho usiwe wa kidanganyifu kwa mtazamaji au kujaribu kujificha na/au

kupotosha ukweli wa ulimwengu asilia;

(ii) taarifa za manukuu zinazotolewa lazima ziwe kamili, za kweli na sahihi; na

(iii) picha hazipaswi kuonyesha wanyama waliokamatwa, fungwa, tawaliwa kwa hila, sanamu za wanyama, ngozi ya wanyama nzima zilizojazwa vitu kurudisha ufanano wa mnyama hai na/au mnyama mwingine yoyote anayenyonywa kwa faida. Isipokuwa, wakati wa kutolea taarifa suala maalum juu ya namna wanyama wanavyofanyiwa na mtu fulani, katika hali ambako lazima uelezee kwa dhairi kwamba mnyama alikuwa amekamatwa, amefungwa, amezuiliwa, ni sanamu au ngozi ya mnyama iliyojazwa vitu kuifanya ionekane ni mnyama hai.

(3) Haupaswi kufanya kitu chochote kuumiza au kufadhaisha mnyama au kuharibu makazi yake katika kujaribu kupata picha. Hii ni pamoja na kupita juu ya mnyama kwa kuruka angani na ndege (au kijindegemvumo) kwa chini sana au kwa kelele - ustawi wa mnyama lazima uwe na kipau mbele.

(4) Unawajibika kuhakikisha utekelezaji kamili wa sheria yoyote inayotumika kitaifa au kimataifa (pamoja na zinazohusiana na za vijindegemvumo) na kupata vibali vyovyote vinavyohusika (ambavyo, ikiwa ni picha za wanadamu, itajumuisha idhini ya mhusika) na ambavyo lazima tuweze kuviona kama tukiviomba.

(5) Kuweka chambo cha moja kwa moja hairuhusiwi, wala njia yoyote ya chambo ambayo inaweza kumweka mnyama hatarini au kuathiri vibaya tabia yake, ama moja kwa moja au kwa kutojali kuwa matendo yanajengea mazoea mnyama. Njia nyingine zozote za kuvutia, ikiwa pamoja na mbegu kwa ndege au kwa harufu, lazima zitolewe taarifa katika manukuu kwa ajili ya kupitiwa na baraza la waamuzi na sisi.

(6) Ikiwa tunashuku kwamba wasilisho limepatikana kwa matendo ya kikatili au yasiyo ya kimaadili, ikiwemo pamoja na matumizi ya chambo ya moja kwa moja au ya kutojali au kwa njia yoyote kukiuka Masharti haya, uwasilisho utafutwa na tunahifadhi haki ya kutaarifu kwa mamlaka husika juu yako.

5. AINISHO ZA PICHA

(1) Uwasilishaji lazima uwe katika muundo wa dijital lakini wasilisho la asili hali hitaji kuwa limepigwa kwa kutumia kamera ya dijitali. Tambazo za ubora wa hali ya juu za angavu au za negativu za picha pia zinakubalika.

(2) Faili za kidijitalii lazima ziwasilishwe kama JPEG, zilizohifadhiwa katika mipangilio ya ubora wa hali ya juu wa angalau 8 katika Photoshop, Adobe RGB (1998), na kwa pikseli 1920 kwa upande urefu mrefu zaidi kwa kategoria zote. Mipaka, taswira fifi au saini visijumuishwe.

(3) Ikiwa picha yako itawekwa kwenye orodha teule utahitaji kutoa yafuatayo:

(i) Faili RAW (kwa mfano .CR2, .NEF, .ORF, .PEF n.k.), au JPEG asilia ambazo hazijaguswa (na anuwai ya faili za "kabla" na "baada" za JPEG ambazo hazijaguswa zitakazo bidi ziwasilishwe kama zikiombwa); na angavu au negativu asilia, zitahitajika kwa uthibitishaji. Faili za DNG zinaruhusiwa tu ikiwa ndio muundo wa RAW asilia wa kamera;

(ii) Faili za mwonekano wa juu (ikiwezekana TIFF) zinazohitajika kwa uchapishaji zinapaswa kuwa 8-bit, Adobe RGB (1998) kwa mwonekano mzima, na zilingane na rangi na upunguzaji wa JPEG uliowasilishwa katika shindano. Tafadhali usiongeze ukubwa. Faili zisizidizidi 500MB.

(4) Uwasilisho wowote ambao hauwezi kuthibitishwa au sio wa ubora unaokubalika utafutwa. Tunahifadhi haki ya kukuomba uwasilishe anuwai ya faili za "kabla" na "baada" za picha yoyote ambayo inahitaji uthibitishaji zaidi.

(5) Marekebisho ya kidijitali ikiwa ni pamoja na rangi/toni na ulinganuzi, kuchoma, kukwepa, kukata, kunoa, kupunguza kelele, kazi ndogo ya kusafisha (kwa mfano uondoaji wa vumbi la kihisio au mikwaruzo kwenye angavu / tambazo, kuondolewa kwa upotovu utokanao na rangi kutolengeka vizuri), HDR, panorama zilizounganishwa, picha zenye mchanganyo wa lengo anuwai vinaruhusiwa ilimradi vinazingatia kanuni za Shindano juu ya uthabiti - uwakilishi wa kweli wa ulimwengu asilia - ili visidanganye mtazamaji au kupotosha ukweli wa ulimwengu asilia, au kile ambacho kilinaswa na kamera hapo mwanzo.

(6) Marekebisho yafuatayo ya kidijitai - lakini bila kukomea kwa haya - hayaruhusiwi: kuongeza, kuhamisha au kuondoa vitu, wanyama au sehemu za wanyama, mimea, watu na kadhalika; kuondoa uchafu, mwangazio, utenganishonyuma, viputo, uchafu na vingine kama hivyo; picha zilizochanganywa kuwa moja, uchoraji mandharimbele/ uchoraji mandharinyuma.

(7) Taarifa za manukuu lazima ziwe kamili, za kweli na sahihi na zijumuishe maelezo juu ya mwenendo ulioonwa; chanzo cha hadithi; eneo hasa; kama chambo kilitumiwa, na kama ni hivyo, cha asili gani (angalia kifungu cha 4.5); na kama spishi hiyo ina umuhimu wa kisayansi.

(8) Haupaswi kuingiza jina lako kwenye manukuu au kwenye picha yenyewe.

6. UAMUZI, TUZO NA ZAWADI

(1) Jopo la wataalam linalojumuisha mwenyekiti na majaji ('Baraza la Waamuzi”') litateuliwa na sisi ili kuchagua na kuzipa tuzo takriban wasilisho mia moja (100) kutoka kwenye Mashindano ya Watu Wazima na Vijana kwa ujumla.

(2) Baraza la Waamuzi litazingatia picha hizo kulingana na vigezo vya uchaguzi vinavyojumuisha uasilia, simulizi na desturi za kimaadili na itapendelea picha ambazo hazijapewa tuzo katika mashindano mengine ya kimataifa inamaanisha mshindi, mshindi wa pili, anayepongezwa, pongezi ya heshima n.. Baraza la Waamuzi itawekwa litatolewa kwenye tovuti ya Shindano hapa.

(3) Wakati wa maamuzi na kwa idhini yetu dhairi, Baraza la Waamuzi linahifadhi haki ya:

(i) kuhamisha wasilisho kutoka kategoria moja hadi nyingine pale inahusu na kufaa;

(ii) kutotoa tuzo katika kategoria fulani kwa njia iliyoelezewa katika kifungu cha 6 (4) hapa chini; au

(iii) kuondoa kategoria nzima yote.

(4) Kutoka kwenye mawasilisho yaliyochaguliwa na Baraza la Waamuzi kutoka kwenye Shindano la Watu Wazima, tuzo zifuatazo zitatolewa ("Tuzo"):

(i) Kategoria ya Lililopongezwa Sana;

(ii) Kategoria ya Mshindi; na

(iii) Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka.

(5) Washindi wa Kategoria tu ndio watazingatiwa na Baraza la Waamuzi kwa tuzo ya Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka. Baraza la Waamuzi linahifadhi haki ya pia kujumuisha kwa ajili ya kuizingatiwa picha moja (1) waliyochagua ya Mshindi wa Kategoria ya kila mojawapo ya kategoria nyingi zifuatazo za picha:

(i) Tuzo la Uandishi wa Habari Kupitia Simulizi kwa Picha;

(ii) Tuzo la Nyota ya Kesho (kati ya umri wa miaka 18 hadi 26); na

(iii) Tuzo la Jalada la Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu (umri wa miaka 27 na zaidi).

(6) Picha nyingine ishirini na tano (25) kutoka Awamu ya Mwisho ya Shindano la Watu Wazima na Shindano la Vijana zitachaguliwa na sisi na kuweza kupatikana kwa umma kwa miezi mitatu (3) kwa ajili ya kupigiwa kura mtandaoni. Mawasilisho haya yatafanyiwa matangazo hasa kupitia mitandao ya kijamii na kupitia wabia wetu wowote wa magazeti au wa kibiashara. Uwasilisho utakaopigiwa kura nyingi zaidi utapokea Tuzo Maalum la Chaguo la Watu, na mawasilisho manne (4) yafuatayo kwa kupendwa sana yatapongezwa sana. Pamoja na hayo, mshindi wa Tuzo Maalum la Chaguo la Watu hatazingatiwa kwa Mpiga Picha wa Viumbe-mwitu wa Mwaka.

(7) Ukifanikiwa, utaarifiwa kwa usiri sana. Hili ni sharti la kuwasilisha katika Tuzo lolote na zawadi yoyote kwamba haufichui maelezo juu ya mawasilisho yaliyo kwenye orodha teule au yanayoshinda kwa mtu yeyote mwingine.

(8) Orodha ya zawadi inapatikana kwenye tovuti. Haiwezi kuhamishwa. Tunahifadhi haki, kwa hiari yetu, kubadilisha zawadi yoyote iliyoorodheshwa, yote au sehemu yake, na zawadi mbadala yenye thamani ya kifedha au ya utangazaji sawa (lakini hautakuwa na haki yoyote ya kudai hili). Tafadhali zingatia kwamba zawadi lazima zidaiwe ndani ya mwaka mmoja wa kutaarifiwa juu ya mafanikio, au ambapo ni zawadi yenye tarehe maalum ya tukio iliyopangwa basi hadi mwezi mmoja (1) kabla ya tarehe hiyo ya tukio, au kwa kila hali itafutwa (pamoja na haki yoyote ya kupokea zawadi au utangazaji wowote mbadala).

7. UTANGAZAJI

(1) Unakubali kwamba, ikiwa kiingilio chako kitachaguliwa na Baraza la Waamuzi utashiriki kwa kiwango kinachofaa cha utangazaji unaohusiana na ukubali matumizi ya jina lako na sura yako kwa madhumuni ya kutangaza, kukuza na utangazaji wa Mashindano na / au Maonyesho ya WPY na / au Maonyesho yoyote yanayohusiana bila fidia ya ziada.

8. HAKI YA MALI YA AKILI NA LESENI

1) Picha yoyote unayowasilisha kwa shindano lazima iwe:

(i) kazi yako ya asili; au

(ii) iliyowasilishwa na wewe kwa niaba ya mpiga picha, katika hali hiyo lazima utujulishe jina la mpiga picha na ukiombwa na sisi lazima utoe uthibitisho wa kimaandishi kutoka kwa mpiga picha kuwa unaidhini ya kutenda kwa niaba yake na kwamba yeye mwenyewe anakubali kabisa na kuwajibika na Masharti haya zenyewe.

(2) Lazima uwe mmiliki pekee wa hakimiliki katika (ma)wasilisho au uwe umepata idhini ya kimaandishi ya mmiliki wa hakimiliki au wamiliki wowote wa pamoja wa hakimiliki kuwasilisha uwasilisho kwenye Shindano. Nakala ya idhini yoyote kama hiyo ya kimaandishi lazima ifikishwe kwetu pale utakap thibitishiwa kwamba picha yako imewekwa kwenye orodha teule kwa ajili ya Tuzo.

(3) Umiliki wa hakimiliki katika uwasilisho wowote uliowasilishwa kwenye Shindano utabaki na wa/mmiliki wa hakimiliki.

(4) Kwa kuzingatia nafasi ya kushinda Tuzo kwa picha unayowasilisha kwa Mashindano, unatupatia sisi na Makumbusho haki ya kuzaa tena, kutangaza na kuonyesha picha hizo kwa njia yoyote (pamoja na lakini sio kwa nakala halisi. , nakala za elektroniki na kwenye media ya kijamii) kuiwezesha kuhukumiwa kwa Tuzo na Baraza la Waamuzi au kura ya umma.

(5) Ni kuhusiana na picha yoyote unayowasilisha ambayo inashinda Tuzo, inayozingatiwa kushinda Tuzo na isiyohitaji kulipiwa nyongeza yoyote isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo, ndio unatuidhinisha sisi, Jumba la Makumbusho, na ikiwa lazima mawakala wowote wanaotenda kwa niaba yetu, haki wakati wa Kipindi cha Leseni:

(i) kutoa upya na kuonyesha picha katika Maonyesho yoyote kwa chapa au kidijitali:

(ii) kutumia picha hiyo katika muundo wowote (iliyofafanuliwa katika kifungu cha 8 (12)) kutangaza na kukuza Mashindano yoyote au Maonyesho, bila malipo zaidi kasoro kama imeelezwa katika kifungu cha 8 (5) (v) hapa chini;

(iii) kutoa kibali tegemezi kwa Wa/Mdhamini Rasmi kutumia picha hiyo ili kutangaza na kusherehekea Shindano au Maonyesho ya WPY na uhusiano wao nao kwa njia yoyote (iliyofafanuliwa katika kifungu cha 8 (12));

(iv) kutoa kibali tegemezi kwa Ziara ya Maonyesho au mwendeshaji ("Mmiliki Leseni ya Ziara ya Maonyesho") kuchapisha au kuandaa uchapishaji wa picha yako kwa maonyesho katika ukumbi wao wa Ziara ya Maonyesho, onyesha picha yako katika ukumbi wa Ziara ya Maonyesho kwa chapa au kwa kidijitali na kutangaza na kukuza Ziara yao ya Maonyesho kwa njia yoyote (iliyofafanuliwa katika kifungu cha 8 (12)); na/au

(v) chapisha picha yako katika Kitabu cha Jalada cha kila mwaka au Kitabu cha Viangazio. Uamuzi wowote wa kutumia haki hiyo utakuwa kwa hiari ya Jumba la Makumbusho lakini ikiwa itatumika basi, Jumba la Makumbusho litakulipa ada ifuatayo: ukurasa wa mbele wa jalada £250.00; ukurasa wa nyuma wa jalada £150.00; matoleo ya ushirikiano ukurasa wa mbele wa jalada kama haujatumika bado kwenye toleo la Uingereza £120.00; matoleo ya ushirikiano ukurasa wa mbele wa jalada kama haujatumika bado kwenye toleo la Uingereza £75.00; Viangazio ukurasa wa mbele wa jalada £150.00; picha moja moja £75.00 (zinaweza kutumika katika Jalada na Viangazio kwa ada moja); Jalada, ‘Nyota ya Kesho’ na simulizi za Uandishi wa Habari kwa kutumia picha £375.00 kwa mkusanyiko.

(6) Fursa zingine za kibiashara zinaweza kupatikana kwako ili ufaidike kutokana na matumizi ya wasilisho lolote lilichochaguliwa na Baraza la Waamuzi. Pale mbapo faida kama hiyo ya kibiashara inaweza kutokea, tutatafuta idhini yako mapema na kukupa leseni inayofaa. Mifano ni pamoja na:

(i) kujumuishwa katika uongezaji soko kwa kutumia alama bainifu unaohusishwa na Shindano, au Maonyesho yoyote, kasoro ya Kitabu cha Jalada na kitabu cha Viangazio; na

(ii) kutoa leseni ya uongezaji soko kwa kutumia alama bainifu kwa mtu mwingine.

(7) Kipindi cha Leseni:

(i) kitaanza tarehe utakapoarifiwa juu ya Tuzo lako na kuendelea kwa kipindi cha miaka mitano (5); na

(ii) baada ya kipindi tajwa Jumba la Makumbusho litahifadhi nakala za picha (elektroniki au vinginevyo) lakini zitatafuta idhini yako ikiwa tunataka kutumia picha hizo kwa madhumuni zaidi.

(8) Sisi, Jumba la Makumbusho na mashirika yoyote yaliyo na leseni chini ya kifungu cha 8 (5) tutakupa sifa, au (kama tofauti) mpiga picha, wakati tunatumia picha kulingana na Masharti haya. Pamoja na hayo, unakubali, kwamba hatutawajibika kwako, au (kama tofauti) mpiga picha, ikitokea bila kukusudia kukosa kuonyesha sifa hiyo.

(9) Ni jukumu lako kuhakikisha kwamba:

(i) picha zozote unazowasilisha zimepigwa kwa idhini ya:

a. mtu yeyote anayetambulika katika picha hiyo; au

b. idhini ya mzazi / mlezi wake ikiwa kama yuko chini ya miaka 16, na

(ii) kwamba watu hao wameshauriwa:

a. kwamba picha inaweza kuwasilishwa kwenye Shindano; na

b. kwamba picha yake inaweza ikatumika kufuatana na Masharti haya.

(10) Unakubali kwamba uwasilisho kwenye Shindano hautoi haki zozote kuhusiana na majina, nembo au mali ya akili yoyote inayohusiana au inayomilikiwa nasi, Jumba la Makumbusho au Shindano. Unakubali kutotoa tamko lolote hadharani kwa kutumia majina, nembo au mali za akili hizo zozote bila idhini yetu ya kimaandishi ya awali.

(11) Tutakumbusha umma kuwa hakimiliki ya picha za Maonyesho zinabaki kwa wapiga picha na hatutahimiza umma moja kwa moja kuchapisha picha za Maonyesho kwenye akaunti zao za kibinafsi za mitandao ya kijamii. Hata hivyo, unatambua kwamba sisi wala Makumbusho, wala Wamiliki wa Leseni za Ziara ya Maonyesho tuna uwezo wa kikweli kweli wa kuzuia hali hii kutokea. Una samehe haki yoyote ambayo unaweza kuwa nayo (kama ipo) ya kuleta madai dhidi yetu, Jumba la Makumbusho au Wamiliki wa Leseni za Ziara ya Maonyesho ikiwa kama matokeo ya kushindwa kuzuia umma kupiga au kushiriki picha za Maonyesho.

(12) Histilahi ya "njia yoyote" inapotumika katika kifungu cha 8 (5) itajumuisha lakini sio tu chapa, kitabu, jarida, wadau wa mawasiliano wa NHM, (media za kidijitali, programu au idhaa za mitandao ya kijamii) wowote.

9. DHIMA

(1) Uthibitisho wa uwasilishaji wa kielektroniki sio ushahidi wa kupokelewa nasi.

(2) Hatuwezi kuwajibika kwa ajili ya barua pepe ambazo hazifiki kwa sababu ya mipangilio yako ya usalama wa barua pepe au vizuizi vilivyowekwa na Mtoa Huduma wako wa Mtandao. Lazima uhakikishe kuwa mipangilio yako inakubali barua pepe kutoka kwa wildlifephotographeroftheyear@nhm.ac.uk na msonlineservicesteam@microsoftonline.com.

(3) Wasilisho za kidijitali kwenye Shindano hazitahifadhiwa au kurudishwa na sisi baada ya majina ya wapiga picha waliopewa tuzo kutangazwa

(4) Kasoro pale ilipoelezewa dhairi sehemu nyingine katika Masharti na kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria, hatutawajibika kwa hasara au uharibifu wowote utakaokabiliana nao kuhusiana na Shindano, matumizi ya uwasilisho lako kulingana na Masharti haya au matumizi ya zawadi yoyote. Kinga hii ya dhima itajumuisha lakini sio tu dhima dhidi ya hasara yoyote au uharibifu kwa uwasilisho wowote, dhima dhidi ya utumiaji mbaya wa picha; na/au kushindwa kwa mmiliki mwingine yeyote wa leseni kutii majukumu ya mikopo katika Masharti haya.

10. ULINZI WA DATA

Tutakusanya data zako za kibinafsi (na za mzazi/ lezi wako pale inapofaa) wakati wa usajili, na kama ilivyoonyeshwa vinginevyo ili kusimamia Shindano, Maonyesho na/au shughuli hususan. Kwa taarifa zaidi juu ya jinsi sisi na Jumba la Makumbusho tunavyochakata data za kibinafsi tafadhali angalia Ilani yetu ya Faragha hapa https://www.nhm.ac.uk/about-us/privacy-notice.html.

11. MATUKIO NJE YA UWEZO WA KAWAIDA WA MMILIKI

Hatukuwa tumekiuka Masharti haya wala hatutawajibika kwa kuchelewesha kutekeleza, au kutotimiza majukumu yake yoyote chini ya Masharti haya ikiwa kuchelewa huko au kutotimiza kunatokana na matukio, hali au sababu zilizo nje ya uwezo wetu wa kawaida. Katika hali kama hizo, tutakuwa na haki ya kuwa na muda wa nyongeza wa kiasi kilicho cha sawa kwa ajili ya kutekeleza majukumu kama hayo. Ikiwa kipindi cha kuchelewa au kutofanya kazi kinaendelea kwa wiki 1, tunaweza kusitisha mkataba na wewe ulioundwa na Masharti haya kwa kukupa ilani ya siku 14 kwa maandishi.

12. MKATABA WOTE

Masharti haya na tovuti au hati nyingine zilizojumuishwa vinafanya sehemu kamili ya mkataba kati yako na sisi na huchukua nafasi na kubatilisha mikataba ya awali, ahadi, dhima, dhamana, uwakilishi na uelewa kati yao, iwe vya maandishi au mdomo, inayohusiana na mada yake, ikiwemo lakini sio nyaraka za matangazo au ukuzaji. Unakubali kuwa hautakuwa na suluhu kuhusu tamko, uwakilishi, ahadi au dhamana yoyote (iwe imetolewa kwa kutojua au kwa uzembe) ambayo haijawekwa katika Masharti haya.

13. HAKI ZA MTU ALIYE NNJE YA MAPATANO HAYA

Zaidi ya haki zilizotajwa dhairi zinazohusu sisi, Jumba la Makumbusho, Wa/Mfadhili Rasmi au Wa/Mmiliki Leseni za Ziara ya Maonyesh, mkataba na leseni iliyokuwepo kutokana na uwasilishaji kufuatana na Masharti haya havitoi haki kwa mtu mwingine chini ya Sheria ya Mikataba (Haki za Mtu Wengine) ya 1999 [Contracts (Rights of Third Parties) Act 1999] ili kutekelezesha vifungu vyovyote vya Masharti haya.

14. SHERIA NA MAMLAKA

Masharti yatasimamiwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Uingereza na Wales na wahusika watawajibika chini ya mamlaka peke ya mahakama za Uingereza na Wales.